Monday, October 8, 2012

Siasa za Libya

Waasi wa Libya waliomng'oa Gadafi madarakani

Bunge la Libya lenye wajumbe 200 lilikataa orodha ya mawaziri aliyopendekeza mwisho wa juma lilopita, na sasa linazingatia orodha mpya.
Tangazo hilo halikutarajiwa, lakini inaelekea limewapendeza Walibya kwa sababu linafuata matakwa yao.
Waziri Mkuu mteule wa Libya, Mustafa Aboushagour, amependekeza baraza la dharura la mawaziri 10 tu, ikilinganishwa na 29 alilopendekeza juma lililopita.
Alisema hilo ni pendekezo la kuongoza Libya bila ya kufikiria majimbo.
Nchi inakabiliwa na changamoto hatari, alisema Bwana Aboushagour.
Iwapo orodha hiyo mpya piya itakataliwa na bunge, basi waziri mkuu itambidi kujiuzulu.
Baada ya kushindwa mara ya kwanza waziri mkuu alivishauri vyama na akaona kila kimoja kinavutia kwake kwa kudai wizara nyingi.
Bwana Aboushagour amesema hatakubali shinikizo.
Matokeo na yawe vyovyote vile, msimamo wake unaweza kuleta mabadiliko katika siasa changa za Libya.

No comments:

Post a Comment

This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people