
Mbunge Sheikh Mohammad Dor alisema
kuwa anajitolea kufadhili vuguvugu la MRC linalotaka kujitenga kwa eneo la
Pwani.
Hatua ya kushtakiwa kwa Sheikh
Mohammed Dor inakuja siku tatu baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa kundi hilo
Omar Mwamnuadzi.
Sheikh Dor alikamatwa jana jioni
baada ya kutangaza hadharani kuwa anaweza kufadhili vuguvugu hilo, ingawa
aliachiliwa asubuhi ya leo kwa dhamana ya dola 23,000 baada ya kukana mashtaka
ya uchochezi.
Wanachama wa MRC wanaotaka kujitenga
na Kenya
Kesi yake itaanza kusikilizwa tarehe
kumi na tatu mwezi Novemba.
Sheikh Dor ambaye amelaani msako
unaoendelea wa polisi dhidi ya kundi hilo mjini Mombasa, alisema kuwa kundi
hilo ambalo mahakama ilisema kuwa sio haramu, kwa mtu kuamua kulifadhili sio
kosa.
Dor ni mmoja wa wabunge kumi na
wawili wa Kenya ambao hawakuchaguliwa ingawa waliteuliwa kuwakilisha maswala
kadhaa bungeni.
Picha na Habari BBC
Picha na Habari BBC
No comments:
Post a Comment
This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people