Monday, January 14, 2013

Lady Jaydee amaliza safari yake ya Kupanda Mlima Kilimanjaro na kampuni ya Kilidove Tours

 A group photo at Marangu gate just after arrival from the 6days Kilimanjaro climb
Lady Jaydee being interviewed by local media
 Kilimanjaro National Park staffs and Kilidove Tours crew posing for a photo after Lady Jaydee finished her six days Kilimanjaro climb which were arranged and organized by Kilidove Tours
 Lady Jaydee with the guides(Gastor left and Deo right) who guided her to Uhuru Peak 5895m at the main Marangu exit gate
Lady Jaydee receiving 'just done Kilimanjaro' souvenir T/Shirt from the managing director of Kilidove Tours and Safaris Ltd after completing her six days Kilimanjaro climb
Lady Jaydee being interviewed by local medias


 Gadner signing guest exit book after completing their six days Kilimanjaro climb
 Lady Jaydee receiving her Mount Kilimanjaro climb certificate from Kinapa chief park warden Mr. Erastus Lufungilo

 Mount Kilimanjaro national Park chief park warden Mr. Erastus Lufungilo signing Mount Kilimanjaro success certificate
We are proud of our team led by head guides Deo Sosta, and Gastor Mosha for amazing job in guiding Tanzania's top celebrity to Africa's highest point.
 Lady Jaydee being the first top celebrity from East Africa to climb mount Kilimanjaro she expressed her feeling and described it as one of the biggest achievement ever in her life. She also added that she will do the best she can to be a good ambassador of Tanzania's beauty and nature
 Lady Jaydee was accompanied by her husband Gadner G Habash who is also a famous radio presenter in Tanzania and a cameraman Justin Bayo together they all made it to Uhuru Peak on 11th Jan 2013

Source: Kilidove Tours blog

Thursday, January 10, 2013

Maendeleo ya Msanii Lady Jaydee katika safari yake ya kupanda mlima Kilimanjaro



 Lady JayDee, Justin Bayo(cameraman) and Gastor(guide) walking towards Mandara Hut

 Gadner,  na Lady Jaydee heading towards Mandara Hut


 A group photo at Mandara Hut with Kinapa Staffs
 Lady Jaydee
 Gadner G Habash




 Lady Jaydee at Zebra rocks


 From left Justin(cameraman), Lady Jaydee(center) and Gadner


 Jide Rock


 From front Gadner, Gastor(guide), Jay Dee, and Deo(guide)


 Jay Dee at caves
And here she comes an iron lady

Progress:
8th Jan - Mandara Hut(2700m) to Horombo Hut(3720m)
Walking hours; 5hrs
9th Jan - Acclimitization Day at Horombo Hut
Walking hours; 4hrs
10th Jan - Horombo Hut(3720m) - Kibo Hut(4703m)
Walking hours; 5hrs
Later in the day they will start heading towards Uhuru Peak(5895m) through Gillman's point(5685m)

Health
Gadner, Lady Jaydee and their cameraman Mr. Justin are in good shape, strong and able to continue till next destinations
Source: Kilidove Tours and Safaris Ltd Blog

Tuesday, January 8, 2013

Lady JayDee apanda mlima Kilimanjaro

Tanzania’s top celebrity Judith Wambura ‘Lady JayDee’ today will follow a chain of world’s top celebrity by climbing Mount Kilimanjaro Africa’s highest point and the world’s free standing mountain through Marangu Route.  As it is known for years Mount Kilimanjaro is one of the world's most famous mountain of which many celebities have conquered including Roman Abrahimovich, Jessica Biel, Justin Timberlake, Lupe Fiasco, Jimy Carter, JBL, and many more

 A six days trek was organized by a local Mount Kilimanjaro experts ‘Kilidove Tours and Safaris Ltd’ of Arusha Tanzania, during her trek she will be assisted and guided by a team of long time experienced and reputable mountain tour guides Gastor Mosha and Deogratias Sosta who also climbed Mount Everest earlier last year for his career.

Along she was joined by her cameraman Justin Bayo, her husband and a famous Radio presenter Gardner G Habash

Prior to departure she said one of her biggest and longest dream was to climb and reach top of Kilimanjaro which is Africa’s highest point at 5895metres
all the best ‘Lady JayDee’


 Lady JayDee(center) Deogratias(right) and Gastor(left) who will guide Lady Jaydee to the Uhuru Peak 5895m
 Lady Jaydee with her cameraman Mr. Justin Bayo at Marangu main entrance gate today

Lady Jaydee and Gardner after signing guest's book at the main entrance gate of Marangu today
 Lady Jaydee at the Park's headquarter main entrance
 Lady Jaydee signing a guest registration book before she starts her trekking
 The crew preparing for set off
 Mount Kilimanjaro chief park warden Mr. Erastus Lufungilo greeting Lady Jaydee before she starts her six days trek
 A team group photo from left Deogratias(guide), Justin Bayo(cameraman), Gardner G Habash(her husband), Gastor(guide) Lady Jay Dee, George(Kilidove Tours) Emanuel(porter) and Mr Erastus Lufungilo(chief park warden)
Lady Jaydee at chief park warden office before setting off for her scheduled Mount Kilimanjaro climb

Friday, December 21, 2012

Raisi Kikwete akutana na uongozi wa club ya Sunderland


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi toka kwa mmiliki na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short huku Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband na Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Bw. John Farnan wakiangalia baada ya mkutano wa na Rais Ikulu jijijni Dar es salam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short huku Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband na Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Bw. John Farnan Ikulu jijijni Dar es salam.

Breakind News: Lema ashinda kesi ya Ubunge sasa kurudishiwa ubunge wake


Hatimaye aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini amerudishiwa Ubunge wake na ndiye mbunge halali wa Chadema Arusha mjini

Hukumu ya Lema ni leo


HOJA tatu za msingi zinatarajiwa kutumiwa na Jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, kuamua rufaa ya kesi ya aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema katika hukumu inayotarajiwa kusomwa leo jijini Dar es Salaam.

Kati ya hoja 18 zilizowasilishwa na upande wa rufaa kupinga hukumu hiyo, zipo hoja tatu ambazo zinaonekana za msingi katika hukumu ya leo itakayotolewa na majaji waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo; Salum Massati, Bernard Luanda na kiongozi wao, Nathalia Kimaro.
Lema alivuliwa ubunge Aprili 5, 2012 katika hukumu iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibalira, kutokana na kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM; Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Kutokana na hukumu hiyo, Lema, kupitia kwa Wakili wake, Method Kimomogoro alikata rufaa Mahakama ya Rufani, akiwasilisha hoja 18 za kupinga hukumu hiyo.

Hoja ya kwanza ni kama mpigakura anaweza kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi kwa niaba ya mgombea husika aliyeshindwa katika kinyang’anyiro cha uchaguzi.
Wakili Mkuu wa Serikali, Timon Vitalis alidai kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilikosea kutengua ubunge wa Lema, kutokana na kesi iliyofunguliwa na walalamikaji wanaodai kuwa ni wapigakura.

Wakili Vitalis, aliyemwakilisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), ambaye pia alikuwa upande wa Lema, alidai kuwa wajibu rufaa hawakuwa na haki ya kufungua kesi kupinga ushindi wa mrufani (Lema) kwa kasoro zilizotokea wakati wa kampeni.

Vitalis alidai kuwa, wajibu rufani hao hawakuwa wahusika katika mchakato huo wa kampeni na hivyo hawakuwa na haki ya kupinga matokeo hayo mahakamani.

Akifafanua zaidi, Wakili Vitalis alidai kuwa anayepaswa kufungua kesi mahakamani kwa madai ya lugha ya matusi ni yule aliyetukanwa kwa kuwa hayo ni maumivu ya mtu binafsi na kwamba hata anapokufa, madai yake nayo hufa wala hayawezi kuendelezwa na mtu mwingine.

“Sasa iweje kwa mtu ambaye yuko hai, lakini watu wengine ndio waje mahakamani kufungua kesi? Alihoji Wakili Vitalis.

Hoja hiyo iliungwa mkono na mawakili wa mrufani, Method Kimomogoro na mwenzake ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.

Wakili Kimomogoro alidai kuwa, Jaji alikosea kuamua kuwa mtu yeyote aliyejiandikisha kupiga kura ana haki isiyo na mpaka ya kufungua kesi kupinga matokeo.
Alidai kuwa, hoja yao ni kwamba mtu anakuwa na haki hiyo pale ambapo haki yake imevunjwa au inaelekea kuvunjwa na si pale aliyeathirika na ukiukwaji wa haki hiyo ni mtu mwingine.

Kwa upande wake, Lissu alidai kuwa mpigakura ana haki ya kupinga matokeo mahakamani kwa madai kuwa haki zake pale ambapo madai yao yanaambatana na haki zilizotajwa kwenye Katiba ambazo ni pamoja na haki ya kupiga kura.

Majibu ya Warufaniwa
Akijibu hoja hiyo, Wakili wa warufaniwa, Alute Mughway alidai kuwa haki hiyo inaelezwa katika kifungu cha 111 (1) (A) cha Sheria ya Uchaguzi (2010) pamoja na Katiba na sheria nyingine za nchi na Kanuni za Maadili ya Uchaguzi zinazokataza siasa za majitaka.
Uamuzi wa Mahakama kuhusu hoja hiyo ndiyo ama utahitimisha hukumu hiyo bila kujadili na kuzitolea uamuzi hoja nyingine, ikiwa mahakama itaamua kuanza na hoja hiyo, au utakaoruhusu kuendelea na mjadala na kisha uamuzi wa hoja nyingine kutolewa.


Ikiwa mahakama itakubaliana na hoja za warufani kuwa katika mazingira ya kesi hiyo, mpigakura hakuwa na haki ya kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo hayo, basi hoja nyingine zitakuwa zimekufa na Lema atarejea bungeni.

Hata hivyo, mahakama haiwezi kufumbwa midomo kuendelea kujadili na kutoa uamuzi kwa hoja nyingine, ikiwa itaona ni vyema kwa lengo la kuweka msingi mzuri na mwongozo katika uamuzi wa mashauri mbalimbali yanayoweza kujitokea baadaye.
Ikiwa mahakama itakubaliana na wajibu rufaa kuwa katika mazingira hayo mpigakura ana haki kupinga mahakamani matokeo hayo, basi mahakama itabidi kuendelee na hoja nyingine.

Hoja nyingine
Hoja nyingine ni matumizi ya lugha za matusi katika kampeni, ambayo ni moja ya hoja za msingi zilizomvua ubunge Lema, baada ya Jaji Rwakibarila kuthibitisha kwamba alimtukana aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk Batilda Burian.

Katika hoja hiyo, Wakili Vitalis alidai kwamba hata kama kulikuwa na lugha ya matusi kama wajibu rufaa walivyodai katika ushahidi wao mahakama haikustahili kumvua Lema ubunge kwa kuwa Bunge liliruhusu matusi kwenye kampeni.

Aliongeza kuwa, kwa mujibu wa Kifungu cha 108 cha Sheria ya Uchaguzi Sura ya 313 ya mwaka 2010, matusi si miongoni mwa mambo ambayo yanaweza kutengua matokeo ya uchaguzi.

Wakili huyo wa Serikali alidai kuwa, Bunge liliruhusu kutukanana baada ya kufanya marekebisho katika sheria ya uchaguzi, mwaka 1995 kufuatia hukumu ya kesi kati ya AG dhidi ya Aman Kabourou.

Alifafanua kuwa awali sheria ilikuwa inaruhusu matokeo ya uchaguzi kutenguliwa kutokana na lugha za matusi, kama ilivyotokea kwa aliyewahi kuwa Mbunge wa Karatu, mwaka 1995.
“Baada ya hukumu ya kesi ya Kabourou, Januari, 1995, mwezi Julai mwaka huo Bunge lilifanya marekebisho na kuondoa suala la matusi katika mambo yanayoweza kutengua uchaguzi,” alidai na kuongeza:

“Hapa Bunge liliifunga mikono mahakama, hakuna kutengua matokeo ya uchaguzi kwa mambo ambayo hayajatajwa. Kwa uamuzi huu waliamua kutukanana, kwa hiyo nasi hatuwezi kuwakatalia”.
Pia alidai kuwa, kifungu cha 108 (2) cha Sheria ya Uchaguzi kinaeleza aina za ubaguzi zinazokatazwa ni pamoja na kidini na kikabila na kwamba aina nyingine kama makazi (Uzanzibar, Ubara) hazijatajwa.
Kuhusu hoja ya matumizi ya lugha ya matusi katika kampeni, Wakili Mughway alipinga madai ya Wakili wa Serikali, akidai kuwa si ya kweli na kwamba alikuwa akiipotosha Mahakama.
“Sikubaliani na maneno ya AG (kupitia wakili wa Serikali Vitalis) kuwa ni ruksa wanasiasa kutukanana,” alidai na kusisitiza kuwa madhumuni ya kukataza vitendo hivyo ni kudumisha siasa safi na kuhakikisha nchi inatawaliwa na siasa safi.
Mbali na hoja hizo, zingine zinazoweza kutumika na majaji hao kutoa hukumu hiyo ni madai kuwa Jaji alitumia ushahidi wa mdomo bila kuungwa mkono na ushahidi mwingine na kwamba aliegemea ushahidi wa walalamikaji na mashahidi wao tu.

Thursday, December 20, 2012

Hoteli za Double Tree by Hilton, Giraffe View zafungiwa kwa uchafuzi wa mazingira



Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa (katikati) akitoa amri ya kuifunga hotel ya Double Tree kutokana na kutiririsha maji taka baharini. Wa kwanza kushoto ni Bw. Karim Kanji – Mkurugenzi Mkazi wa hotel hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa (wa kwanza kulia) akikagua mfumo wa maji taka katika Hotel ya Double Tree jijini Dar es Salaam. Kulia kwa Waziri ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Kitwana na Dkt. Robert Ntakamulenga kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Hotel ya Double tree iiliyofungiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, kutokana na kutiririsha maji taka baharini. Hotel hiyo imefungwa rasmi jana.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEghrXEhH2Vm5KyIiTql4751G4LUSe8MblcbXYUDdgRn3Ffe0UGDHlnCJ4Yug8LnFp2wj255MVbuS2exHc3wGHBTlc0-FOpIGwLRHewxVP48tnQp1fVJCVQeja4kJMLBxIoB11hiZ0O320dN/s1600/_DSC0190.JPG
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu mazingira Dr. Terezya Huvisa akitoa amri ya kuifungia hoteli ya Giraffe ocean view iliyopo jijini Dar es Salaam alipozitembelea kukagua hali ya mazingira
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh9N5qY7jtoBl20mbkfpfCLjaHtjSXoC79Q1F0uUvGVqccE7RHSFe_qhyju-wASdIxOfbLgCA6LHkn5Fs8sRcgXEkGZ_-S9VX0l-qW2ACcH5kYR9S98DL4Y6zT4amzWP_BDBZNSTY0lnPz1/s1600/_DSC0109.JPG 

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh6gPu9jrEgPdZA5ARQ_ya-wBULPfrYfK2U2jzUrw5CZCvt_Z9Oj0SKIFYccJTgxkPkBOb_U_x6j7IugY9baZYf-VZMHngT2m520zsWeWhqKBXA_WUKmHHk27gNhxJ3I7mb8DgzSFnxZ2d1/s1600/_DSC0098.JPG 
Na Lulu Mussa na Ali Meja
Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Dk. Terezya Huvisa hii leo ameifungia hotel ya Double Tree na Giraffe Ocean view za Jijini Dar es Salaam kutokana na kutiririsha maji taka baharini.
Waziri Huvisa ametoa agizo hilo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza akiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Charles Kitwanga. 
Ziara hiyo ililenga kuona utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa awali na Naibu Waziri Mh. Charles Kitwanga mapema mwezi huu, alipofanya ziara kutembelea viwanda na hoteli zilizo pembezoni mwa bahari kuona mfumo wa maji taka. 
Katika ziara hiyo, Hotel ya Double Tree iliagizwa kuwa na mpango wa muda mfupi na wa haraka wa kusitisha utiririshaji wa maji taka baharini ambao mpaka leo hotel hiyo ilikuwa bado haijatekeleza. 
Sambamba na hilo na hilo Waziri Huvisa amefuta hati ya ukaguzi wa Mazingira (Environemental Audit) na kuitaka hoteli hiyo kurekebisha mara moja mfumo huo ikiwa ni sambamba na kulipa faini kwa baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).