![]() |
Warembo wakipata mlo wa mchana |
JUMLA ya warembo 29
kati ya 30 wanaowania taji la REDDS MISS TANZANIA 2012 leo wameanza ziara rasmi
ya kutembelea Vivutio vya Utalii vilivyopo Kanda ya Kaskazini katika mikoa ya
Moshi, Arusha na Manyara.
Warembo hao wakiongozwa na Viongozi wa Kamati ya Miss
Tanzania, wakiwa katika mikoa hiyo watatembelea vivutio hivyo na kuhamasisha
jamii ya watanzania kuwa na desturi ya kutembelea vivutio hivyo vyua ndani na
kuhamasisha utalii.
Pia warembo hao watapata fursa ya kujifunza vitu mbalimbali
kuhusiana na masuala ya utalii. Oktoba 7, warembo hao watatembelea Hifadhi ya
Mlima Kilimanjaro, katika lango kuu la kupandia Mlima huo la Marangu.
Aidha kwa mujibu wa ratiba hiyo, inaonesha kuwa warembo hao
watafanya tamasha la Michezo mjini Arusha kabla ya kuelekea Monduli ambako
Oktoba 8 watazuru Kaburi la Waziri Mkuu wa Zamani, Hayati Edward Moringe
Sokoine.
No comments:
Post a Comment
This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people