Sunday, November 4, 2012

Birgitte Alfred ndiye Miss Tanzania 2012/2013

 Birgit Alfred katikati baada ya kutwa taji hilo usiku wa kuamkia leo na kuwamwaga wengine 29


HATIMAYE kile kitendawili cha muda mrefu cha Nani ata twaa taji la Redds Miss Tanzania 2012, kimeteguliwa usiku wa Novemba 3, 2012, baada ya Mrembo kutoka Kitongoji cha Sinza na Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Brigitte Alfred kutwaa taji hilo.

Brigitte ambaye nyota yake katika mashindano hayo ya urembo nchini ilianza kung’aa tangu Kitongoji cha Sinza baada ya kutwaa taji la Sinza na Baade kutwaa Taji la Redds Miss Kinondoni amedhihirisha ukali wake baada ya kuwabwaga warembo wenzake 29 waliokuwa wakiwania taji hilo kutoka Kanda mbambali.

Mpinzani mkubwa wa Brigitte katika shindano hilo alikuwa ni Mrembo kutoka Kanda ya Ziwa ambaye nae alianza kuwika baada ya kutwaa taji la Redds Mkoa wa Mara na baade kutwaa taji la Kanda ya Ziwa, Eugene Fabian.

Enagene alifanikiwa kushika nafasi ya pili katika shindano hilo kubwa ambalo Brigitte ameondoka akiendesha gari aina ya NOAH na kitita cha Shilingi Milioni 8.

Nafasi ya tatu ilikwende kwa Malkia wa Kitongoji cha Kigamboni City na Miss Temeke 2012, Edda Sylvesta huku nafasi ya Nne ikichukuliwa na Mrembo wa Dar Indian Ocean na Kinondoni, Magdalena Roy na nafasi ya Tano ikienda Kanda ya Ziwa tena kwa Mkoa wa Mwanza, Happyness Daniel.










 Mrembo Birgitte akiwa kwenye vazi lake la ubunifu
Rachel wa THT akiburudisha
 Warembo wakiwa kwenye mavazi ya ufukweni

No comments:

Post a Comment

This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people