Wote tunafahamu kuwa aliyekuwa gavana wa benki kuu ya Tanzania Daudi
Balali alifariki dunia tarehe 16.05.2008 huko Boston, Marekani na
kuzikwa huko huko.
Lakini kwa watumiaji wa Twitter watakuwa wanamfahamu Daudi Balali wa
kwenye mtandao huo ambaye ameendelea kumuumiza vichwa vya watu wengi
kuwa ni nani huyu aliye nyuma ya akaunti hiyo na akiendelea kudai kuwa
bado yupo hai?
October 1 alitweet, “Nitakutana na Rais Kikwete na ujumbe wake wiki hii hapa Marekani.
Anavyoonekana ni msomi haswaa na anaishi nje ya nchi. Ni mtu makini, ana
hoja, anaijua siasa ya Tanzania na yupo consistent! Hivi karibuni mtu
huyo alidai kuwa amekuja Tanzania na kulala kwenye hoteli iliyo karibu
na ofisi yake ya zamani.
“In Dar es Salaam, Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kempinski
Kilimanjaro Hotel. Feels good to be close to my former office, BoT,”
alitweet November 13.
Kutokana na kile anachokiandika anaonekana kuwa ni kada mzuri wa CCM
na leo ameibuka na kutabiri anguko la CHADEMA kwa kutweet, “Chadema will
die by disintegration. Zitto Kabwe and 3 other prominent members will
move to CCM,the rest will form 2 new political parties.
Anasema CHADEMA itavunjika ambapo Zitto Kabwe na wanachama wengine
watatu wa chama hicho watahamia CCM na wengi wataanzisha vyama viwili
vipya vya siasa.
Hata hivyo anadai ameamua kuondoka nchini mapema na kurudi Gaithersburg, Maryland kutokana kuhofia usalama wake.
“I am leaving Dar es Salaam tonight instead of Wednesday on security reasons.”
Mwisho ameendelea kusisitiza kuwa kweli yupo hai kwa kutweet:
I AM REAL. TAKE IT OR LEAVE IT. TWITTER IS THE MESSENGER. THE SURPRISE IS YET TO COME.
Ni nani huyu? Anyways, wonders will never cease!!
No comments:
Post a Comment
This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people