Wapalestina 39, wakiwemo watoto kadha, wameuwawa tangu mashambulio hayo kuanza siku ya Jumatano.
Wapiganaji wa Gaza wameendelea kurusha makombora dhidi ya Israil, baada ya kulenga miji ya Tel Aviv na Jerusalem hapo jana.
Hamas imeomba madawa kutoka nchi za Kiarabu.
Israel inasema mashambulio yake yameleta
uharibifu mkubwa katika vituo vilioko chini ya ardhi ambako makombora
ndiko yanakorushwa.
Waziri wa mashauri ya Nchi za Nje wa Tunisia,
ambaye alitembelea eneo la Gaza Jumamosi, alitoa wito kwa viongozi wa
Kiarabu - wataokutana baadae mjini Cairo - kumaliza kile alichoita
uhasama wa Israel.
No comments:
Post a Comment
This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people