Rapper wa kundi la Weusi Lord Eyez leo asubuhi alifikishwa
mahakamani katika mahakama ya wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaa
akitokea mahabusu katika kituo cha polisi cha Oysterbay na kushindwa
kupanda kizimbani baada ya hati ya mashtaka kutokidhi mahitaji ya
kisheria.
Lord Eyez alifikishwa mahakamani hapo majira ya saa tatu asubuhi
katika defender, chini ya ulinzi mkali wa polisi na kupelekwa moja kwa
moja mahabusu akifichwa asionekane hadharani kwa waandishi wa habari
ambao walijazana kwa wingi katika eneo la mahakama hiyo.
Aidha, shauku ya watu wote waliokuwepo mahala hapo ilipotea pale
walipopata taarifa kwamba msanii huyo hatapandishwa mahakamani kwa kuwa
hati yake ya mashataka ilikuwa na makosa tofauti na anayotuhumiwa nayo,
hivyo kuhitajika kufanyiwa marekebisho kabla ya kupelekwa kwa
mwanasheria mkuu na kurudishwa mahakamani kwa ajili ya kupangiwa siku ya
msanii huyo kufikishwa mahakamani tena.
Kutokana na ulinzi mkali, ilikuwa ngumu kupata picha zake.
No comments:
Post a Comment
This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people