Friday, November 23, 2012

Polisi Arusha yaua majambazi


 Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ0 ambazo zilikutwa  kwenye begi la watu watano ambao wanasadikiwa kuwa ni majambazi .Tukio hilo lililtokea katika eneo la Olmatejoo jijini Arusha leo asubuhi na Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwajeruhi kwa risasi Watatu kati yao ambao baadae walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali.Picha na Mahmoud Ahmad-Arusha

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha bunduki zilizokutwa kwenye begi la watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambapo watatu kati yao walijeruhiwa kwa risasi na askari wa jeshi la Polisi na kisha kufariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha kitako cha bunduki aina ya Rifle iliyokutwa kwenye begi la watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi. Watatu kati yao walijeruhiwa kwa risasi na askari wa jeshi la polisi na kisha kufariki dunia leo asubuhi

No comments:

Post a Comment

This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people