UWANJA wa ndege wa kimataifa Jijini Mbeya ulio katika hatua za mwisho za
ujenzi unadaiwa kuvamiwa na watu kutoka nje ya mkoa kwa lengo la
kuwekeza vitega uchumi.
Wavamizi hao wanadaiwa kutoka katika
mikoa ya Kilimanjaro, Arusha,Morogoro na nchi jirani Zambia,Kenya na
Malawi ambao inasemekana kuwa wameanza kujitwalia maeneo yaliyo jirani
na uwanja kwa ajili ya vitega uchumi baada ya kusikia kuwa Serikali ipo
mbioni kufungua uwanja huo.
Katibu wa Madiwani wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Mkoa wa Mbeya, Geofrey Kajigili
alibainisha tukio hilo kwa waandishi wa habari jijini Hapa.
“Nina
uhakika na ninachokisema kwenu na kwamba nina ushahidi wa watu kutoka
Moshi, Arusha na baadhi ya nchi jirani kama Kenya, Malawi na Zambia
ambao wamejitwalia maeneo kwa kuyanunua kutoka kwa wananchi wa eneo hilo
kwa ajili ya kuweka vitega uchumi,” alisema Kajigili.
Kufuatia
kuwapo kwa hali hiyo Kajigili aliwataka wakazi wa mkoa wa Mbeya kuwa
makini na ardhi yao na wasikubali kuiuza ovyo badala yake ndio wajipatie
fursa ya kujiwekea vitega uchumi katika maeneo hayo.
Aidha,
alisema kuwa wakazai hao wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo ya
kufunguliwa kwa uwanja huo wa ndege wa kimataifa kwa ajili ya
kujiendeleza kiuchumi badala ya kuwa watazamaji wa wageni walioanza
kuingia kinyemela katika maeneo hayo.
Mbali na hilo, Kajigili
alisema kuwa Serikali Mkoani hapo inawajibu wa kuwahamasisha wananchi
wake kuwekeza kwenye maeneo hayo kwa kuwa ni fursa muhimu ya uchumi kwa
wakazi hao na sio kuwaachia wageni wanufaike peke yao.
Kwa
mujibu wa Kajigili, Serikali inatakiwa kuwa na mipango ya muda mrefu
kwa kuandaa ardhi ya kutosha wakati huu kwa ajili ya matumizi ya baadaye
badala ya kusubiri wananchi wawekeze na kisha kuwabomolea nyumba zao
pale Serikari inapotaka kutumia ardhi hiyo kwa shughuli nyingine za
kimaendeleo.
No comments:
Post a Comment
This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people