Ufafanuzi kesi ya Dowans
Ufafanuzi kuhusu
gharama za uendeshaji kesi ya Dowans. Juzi kwenye harambee ya M4C nilisema
kwamba kabla ya kwenda Mwanza nilikuwa nafanya mahesabu ya kiwango cha gharama
ambazo TANESCO imetumia na ina mwelekeo wa kutumia kwenye kesi ya Dowans pekee
nikasema ni dola zaidi ya milioni 29 (ambayo ni bilioni takribani zaidi ya 40).
Nitoe ufafanuzi
kwamba katika mahesabu yangu nimejumuisha USD 2.9 ml/- (takribani bilioni 4) za
gharama za mawakili katika mazingira yenye utata. Na gharama za kibenki
iliyowekwa Uingereza katika mazingira ya hatari ya kupoteza (risk) ya dola
zaidi ya milioni 28 (bilioni zaidi ya 40) na gharama nyinginezo ambazo
nitazikokotoa baadaye. Ni vizuri mkarejea hotuba niliyoitoa bungeni tarehe 27
Julai, 2012 ambapo nilitaja namna kesi za Dowans, IPTL, zinavyotumiwa kifisafi
kama vitega uchumi kwa gharama zenye kubebesha mzigo kwa Tanesco na hatimaye
wananchi kupitia bei ya juu ya umeme.
John
Mnyika,
Waziri
Kivuli, Wizara ya Nishati na Madini.
No comments:
Post a Comment
This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people