
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa (katikati)
akitoa amri ya kuifunga hotel ya Double Tree kutokana na kutiririsha
maji taka baharini. Wa kwanza kushoto ni Bw. Karim Kanji – Mkurugenzi
Mkazi wa hotel hiyo.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa (wa kwanza
kulia) akikagua mfumo wa maji taka katika Hotel ya Double Tree jijini
Dar es Salaam. Kulia kwa Waziri ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,
Charles Kitwana na Dkt. Robert Ntakamulenga kutoka Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Hotel ya
Double tree iiliyofungiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais –
Mazingira, kutokana na kutiririsha maji taka baharini. Hotel hiyo
imefungwa rasmi jana.
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu mazingira Dr. Terezya Huvisa akitoa amri ya kuifungia hoteli ya Giraffe ocean view iliyopo jijini Dar es Salaam alipozitembelea kukagua hali ya mazingira
Na Lulu Mussa na Ali Meja
Waziri wa
Nchi wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Dk. Terezya Huvisa hii
leo ameifungia hotel ya Double Tree na Giraffe Ocean view za Jijini Dar es Salaam kutokana na
kutiririsha maji taka baharini.
Waziri
Huvisa ametoa agizo hilo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza akiwa
na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Charles Kitwanga.
Ziara hiyo
ililenga kuona utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa awali na Naibu Waziri
Mh. Charles Kitwanga mapema mwezi huu, alipofanya ziara kutembelea
viwanda na hoteli zilizo pembezoni mwa bahari kuona mfumo wa maji taka.
Katika ziara
hiyo, Hotel ya Double Tree iliagizwa kuwa na mpango wa muda mfupi na wa
haraka wa kusitisha utiririshaji wa maji taka baharini ambao mpaka leo
hotel hiyo ilikuwa bado haijatekeleza.
Sambamba na
hilo na hilo Waziri Huvisa amefuta hati ya ukaguzi wa Mazingira
(Environemental Audit) na kuitaka hoteli hiyo kurekebisha mara moja
mfumo huo ikiwa ni sambamba na kulipa faini kwa baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
No comments:
Post a Comment
This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people