Saturday, October 13, 2012

Breaking News! Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza SACP Liberatus Barlow afariki Dunia





Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza SACP Liberatus Barlow ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanasadikiwa kuwa ni majambazi katika eneo la Kitangili jijini humo usiku wa kuamkia leo
Habari zinasema marehemu aliuawa majira ya saa tisa usiku akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake akitokea kumrudisha dada yake baada ya kuhudhuria kikao cha harusi
Mkuu wa polisi Said Mwema amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari mkuu wa upelelezi makosa ya jinai DCI Robert Manumba akiwa na kikosi cha makachero wameelekeza nguvu zao Mwanza kuongeza nguvu katika upelelezi mkali ambao umeshaanza
Habari zaidi ungana nasi baadaye

No comments:

Post a Comment

This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people