Itakumbukwa kuwa
wakati wa Mkutano wa Nane wa Bunge uliofanyika kuanzia Juni – Agosti, 2012, Spika
wa Bunge aliunda Kamati Ndogo ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kuchunguza
tuhuma zilizokuwepo kuwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na
baadhi ya Wabunge walijihusisha na Vitendo vya rushwa wakati wa mjadala wa
Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini (2012/2013).
Hivyo, Tangazo hili linatolewa kuuarifu
Umma kwamba Kamati hiyo Ndogo imekamilisha kazi yake kama ilivyoelekezwa kwenye
Hadidu za Rejea na kukabidhi Taarifa ya Uchunguzi huo kwa Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano tarehe 27 Septemba, 2012.
Kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge
(2007), Spika atatoa muongozo kuhusu utaratibu wa kufuata kuhusu uwasilishaji
wa Taarifa hii Bungeni ambapo yaweza kuwa Spika akatoa uamuzi ama Kamati
kuwasilisha Taaarifa hiyo Bungeni.
Spika atatoa taarifa ya kukamilika kwa
uchunguzi huo Bungeni wakati wa Mkutano wa Tisa wa Bunge unaotarajia kuanza
tarehe 30 Oktoba, 2012.
Imetolewa na:
Ofisi ya Bunge
S.L.P. 9133
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment
This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people