
Mansoor Yussuf Himid
---
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt Ali Mohammed Shein
amefanya mabadiliko katika Baraza la Mapinduzi. Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi
na Katibu wa Baraza la Mapinduzi,Dkt Abdulhamid Yahya Mzee imesema katika
mabadiliko hayo, Rais Dkt Shein amemteua Shawana Bukheti Hassan kuwa mjumbe wa
Baraza la Mapinduzi.
Rais
Dkt Shein amefuta uteuzi wa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi,Mansoor Yussuf Himid.
Katika uteuzi mwengine Dkt Shein amewateua Mtumwa Kheir Mbarak kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Maliasili na Mohammed Said Mohamed kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.
Katika uteuzi mwengine Dkt Shein amewateua Mtumwa Kheir Mbarak kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Maliasili na Mohammed Said Mohamed kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.
Katika
hatua nyengine, Rais Dkt Shein amefanya mabadiliko ya baadhi ya Makatibu Wakuu
katika Wizara za Miundombinu na Mawasiliano, Wizara ya Ardhi,Makaazi,Maji na
Nishati.
Dkt.
Juma Malik Akili ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano akichukua nafasi ya Dkt. Vuai Idd Lila atapangiwa kazi nyengine.
Ali Khalil Mirza ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati.
Kabla
ya uteuzi huo, Mirza alikuwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii
Zanzibar,aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Mwalimu Ali Mwalimu atapangiwa
kazi nyengine.
Taarifa
ya Ikulu imesema pia Rais Dkt Shein amemteua Tahir M. Abdulla kuwa Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Msanif Haji Mussa atapangiwa kazi nyengine.
Uteuzi
mwengine ni Mustafa Aboud Jumbe ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo alikuwa Tahir M
Abdulla ambaye amehamishiwa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano.
Rais
Dkt Shein ameteua CDR Julius Nalim Maziku kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye anajaza nafasi iliyoachwa wazi na
Kapteni Juma Abdulla Juma ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Bandari Zanzibar hivi karibuni.
Uteuzi
mwengine ni Juma Ameir Hafidh ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais(Fedha,Uchumi na Mipango ya Maendeleo) ambaye amechukuwa nafasi iliyoachwa
wazi na Abdi Khamis Faki aliyeteuliwa kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar.
Aidha,
aliyepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar, Saleh
Ramadhan Ferouz ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar
ambaye
anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Ali Khalil Mirza aliyeteuliwa kuwa Katibu
Mkuu Wizara ya Ardhi, Makaazi,Maji na Nishati.
Pia
Rais Dk Shein amemteua Mussa Haji Ali kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia
Rushwa na Uhujumu uchumi Zanzibar. Uteuzi huo wote unaanza Oktoba 15 mwaka
2012.
No comments:
Post a Comment
This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people