Sunday, October 21, 2012

Freemason Tanzania itakuwa janga la kitaifa


Ndugu,nimekuwa nikiandika kila mara ninapoona ujinga unaoenezwa juu ya freemason.Ingawa binafsi nimekuwa nikikosoa namna watu wanavyobugizwa propaganda zisizo na mashiko juu ya kuwa hiki ni kikundi  cha waabudu shetani na au wachawi,au kuwa wanauwezo wa kumfanya mtu tajiri,bado watu wengi tu wamekuwa wakinipigia simu wakitaka niwasaidie kujiunga na kikundi hicho.Nitumie fursa hii kusema tena kuwa mimi siyo tu siyo mwanachama wa kikundi hicho,bali pia sifahamu namna kinavyopokea wanachama wake.ninachojua na kwa uhakika kabisa sasa ni kuwa wajanja wachache watawaibia wajinga hela zao kwa kuwaahidi uongo mtupu kama kuwaingiza freemason ili watajirike.mfano tangazo hili juu nimelikuta limebandikwa sinza,na namba za simu hizi zinapatikana,najaribu kuona wanachoeleza hawa wapambe wa freemason wanaoweka matangazo.tujuavyo hata kwa kusikia tu ni kuwa chama hiki kinasifika kwa kuwa chama cha siri,nini kimetokea hapa tanzania mpaka kinaweka mabango kualika wanachama? jibu ni rahisi,Tanzania ya siku hizi matapeli ni wengi.wapo watakaotapeliwa kwa mtindo huu wa freemason.
Rwezahura

No comments:

Post a Comment

This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people