Serikali imesema inatambua kwamba Sanaa ni ajira rasmi licha ya kuwa
sekta hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiuratibu, uongozi na
kupewa kipaumbele katika mipango ya kimaendeleo na Serikali.
Akiwasilisha
mada ya Umuhimu wa Tasnia ya Sanaa katika kukuza Ajira nchini, katika
Jukwaa la Sanaa, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Kazi na
Ajira, bwana Haji Janabi amesema sanaa ina mchango mkubwa katika kukuza
na kuendeleza upatikanaji wa nafasi za ajira na kipato.
“Kwa
Tanzania iwapo tutatumia vyema uwepo wa ubunifu muafaka katika sekta ya
sanaa zetu bila shaka tasnia hii inaweza kuchangia sana upatikanaji wa
nafasi za ajira na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuondoa
tatizo la ajira hapa nchini,” alisema Janabi.
Janabi amesema kwamba
pamoja na hivyo kuna changamoyo kubwa ya kiuratibu na kimuundo ikiwa ni
pamoja na Serikali kutotoa kipaumbe katika masuala yanayohusu sanaa na
wasanii pamoja na mgongano wa kimamlaka kati ya vyombo vinavyohusika na
uratibu wa masuala ya sanaa.
Aidha amesema pamoja na nafasi nzuri ya
kukuza ajira, ujio wa teknolojia umeanza kubana soko la ajira ya sanaa
ambapo kwa sasa teknolojia inapunguza uhitaji wa watu katika ufanyikaji
wa sanaa kwa akitolea mfano katika muziki ambapo vitu vingi vinafanywa
na mtu mmoja hivyo kupunguza nafasi za watu wengine.
Pia amesema ili
sekata hii iweze kuwa ajira nzuri zaidi ni muhimu kukaandaliwa viwango
na vigezo kama ilivyo kwa fani zingine ili kuwe na maradaja ya
wafanyaji kazi kulingana na viwango vya umahiri na taaluma.
No comments:
Post a Comment
This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people