![]() |
Jackob Zuma na wake zake |
Tangazo limetolewa na ofisi ya mhifadhi wa masilahi ya wananchi, baada ya magazeti kutuhumu kwamba ukarabati unaopangwa kufanywa kwenye nyumba ya Rais Zuma utaogharimu dola milioni 25, karibu wote unatarajiwa kulipwa na serikali.
Msemaji alieleza kuwa kamati ya uchunguzi imewasiliana na ofisi ya rais kuhusu ujenzi huo kwenye nyumba ya Rais Zuma ilioko Nkandla katika jimbo la KwaZulu-Natal.
Serikali ya Afrika Kusini inasema ujenzi huo unafuata kanuni rasmi.
No comments:
Post a Comment
This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people