MSANII wa muziki wa Zouk mwenye sauti ya kiafrka zaidi Mwasiti, ameanza
kutimiza ndoto zake kwani hivi karibuni amefanya kazi na producer wa
msanii maarufu Akon, ngoma mbili ambazo ni ‘Woman’ na nyingine ambayo
bado hajaipa jina kwani itakuwa ya kiswahili zaidi.
Producer huyo anafahamika kwa jina la Hakim, ndiye aliyeandika ngoma ya
Akon ya ‘Mama Africa’ na kuiandaa katika studio za Konvict pamoja na
ngoma nyingine kibao ambazo zimempa umaarufu.
Akiongea na DarTalk juu ya ishu hiyo aliposema kuwa producer huyo
alikuwa nchini kwa wiki moja kwa ajili ya kutengeneza wimbo maalumu kwa
ajili kombe la afrika, ndipo alipokutana naye ambapo alipata nafasi ya
kuzisikiliza ngoma zake.
Msanii huyo alisema kuwa baada ya producer huyo kusikiliza ngoma zake
akamuuliza swali kuwa anapenda kufanya naye swali ambao Mwasiti aliijibu
kwa furaha kwani malengo yake anaamini sasa yanaenda kutimia.
Hata hivyo alisema ngoma hizo wamefanya na amezichukua kwa ajili ya
kwenda kuzitengeneza na baada ya kukamilika atamtumia, ingawa anaamni
ngoma yake moja ya ‘Woman’, itapigwa sana Afrika kwani amejaribu
kuchangaya lugha mbili kiingereza na kiswahili.
“Yani kwanza siamini kupata bahati ya
kukutana na producer mkubwa kamka huyo ambaye tayari ameshafanya kazi na
wasanii wakubwa ambao wanatamba Afrika na Duniani, hivyo naamini
malengo yangu yatatimia na kufika mbali kwa sababu mara kwa mara
nazungumza na producer huyo na amekuwa akinipa moyo wa kufika,” alisema.
No comments:
Post a Comment
This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people