Tuesday, November 6, 2012

Taarifa toka wizara ya Nishati na Madini

TAARIFA KWA UMMA
Wizara ya Nishati na Madini (MEM)  inapenda kuutangazia umma kuwa Serikali inatarajia kuzindua mradi wa ujenzi wa miundombinu ya kusafisha na kusafirisha gesi asilia kutoka Mnazi Bay Mtwara na Songo Songo Kilwa  hadi Dar es Salaam.

Hafla ya kuweka Jiwe la Msingi wa mradi huo itafanyika tarehe  8/11/2012 Kinyerezi, Manispaa ya Ilala, katika eneo ambapo mitambo ya kuendeshea mfumo mzima wa gesi itajengwa. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Wananchi wote wa Dar es Salaam na maeneo yanayozunguka eneo la Kinyerezi mnaalikwa na mnaombwa kufika kwenye eneo la mradi saa 2.00 asubuhi.

GESI ASILIA KWA MAENDELEO YA TAIFA

Imetolewa na 
Katibu Mkuu 
Wizara ya Nishati na Madini

No comments:

Post a Comment

This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people