Shirika
la Ugavi wa Umeme nchini Tanzania (TANESCO)
limeibuka mshindi wa jumla wa kero kwa wateja wa huduma mbalimbali
na bidhaa hapa nchini kupitia mchakato
unaoendelea kupitia mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook. Nafasi ya pili
ilishikiliwa na Kampuni ya mawasiliano ya Tigo na ya tatu kuchukuliwa na
kampuni ya mawasiliano ya Vodacom.
Katika
mzunguko wa kwanza jumla ya makampuni 29 yaliingia katika kinyanganyiro na kufanikiwa
kuchukua ushindi katika makundi mbalimbali .
Katika
kundi la huduma za usafiri wa Anga , Shirika la Ndege la Precision ndio
liliongoza kwa kero na huduma zisizo na uhakika huku kundi la huduma za maji
likishikiliwa na Dawasco.
Kwa
upande wa usafiri wa mabasi Kampuni ya Happy Nation iliongoza kwa malalamiko
kutoka kwa wateja huku kundi la ving’amuzi vya Televisheni likiongozwa na Star Times.
Kwa
upande wa huduma za maegesho ya magari , eneo la Magogoni Ferry limelalamikiwa
na wateja kwa huduma mbovu na kufanikiwa kushika nafasi za juu katika kundi
hilo.
Kwa
upande wa wateja wanaolipia huduma za Televisheni kituo cha TBC pekee ndicho
kimelalamikiwa kwa kutokuwa na huduma za uhakika kwa watazamaji wake.
Katika
kundi la huduma za mawasiliano ya simu za mkononi , Kampuni ya Tigo ndiyo
iliibuka mshindi ikifuatiwa na Kampuni
ya Vodacom.
Zoezi
hili la kukusanya kero linafanywa na Wananchi kupitia akaunti ya Twitter inayopatikana
kupitia @hudumambayatz na facebook group iliyopewa jina la HUDUMA BONGO ambapo
huduma na bidhaa zote zinazolipiwa na wateja mfano Burudani, Elimu, Hospitali,
Hoteli, n.k zinazowakera wateja zitaingia katika kinyanganyiro hicho.
Washauri
wa kibiashara wa Huduma Bongo wanatoa wito kwa viongozi wa juu wa Mashirika yote
29 yaliyotajwa kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha wateja wao wanapata huduma
bora kulingana na fedha wanazotoa ili kuweza kuleta maendeleo ya Taifa.
Zoezi
hili linaendelea ambapo katika mzunguko wa kwanza jumla ya kero 119
ziliwasilishwa na wateja endapo msomaji una kero iliyoshindwa kupatiwa ufumbuzi
na watoa huduma hawa unahitajika kuwa na akaunti inayotambulika ya Twitter au Facebook
na kujiunga na Huduma Bongo kisha ueleze kero yako. Ukweli na Haki kuzingatiwa.
No comments:
Post a Comment
This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people