
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano, Mhe. Balozi Rajab Gamaha (aliyesimama) akifungua
Mafunzo ya Upimaji wa Utendaji Kazi kwa Uwazi (OPRAS) kwa Wakurugenzi na
Maafisa wa Wizara yaliyoendeshwa na Wakufunzi kutoka Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Wengine katika picha kutoka kushoto ni
Bw. Dushhood Mndeme, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa
Rasilimali Watu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Neema, Mkufunzi
kutoka Utumishi na Bi. Elizabeth Makyao kutoka Utumishi.

Bi. Neema kutoka Utumishi akisisitiza
jambo kuhusu mafunzo hayo kwa Wakurugenzi na Maafisa wa Wizara (hawapo
pichani) huku Balozi Gamaha akisikiliza.

Bi. Elizabeth kutoka Utumishi
akiwasilisha mada kuhusu mfumo huo wa upimaji kazi kwa njia ya uwazi
(OPRAS) kwa Wakurugenzi na Maafisa wa Wizara (hawapo pichani) huku Bal.
Gamaha, Bw. Mndeme na Bi. Neema wakimsikiliza.

Baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia mafunzo hayo.

Baadhi ya Wakuu wa Vitengo na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje walioshiriki mafunzo hayo.

Baadhi ya Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo ya OPRAS.

Maafisa wengine wa Mambo ya Nje wakiendelea na mafunzo ya OPRAS.

Baadhi ya Wakurugenzi na Wakurugenzi
Wasaidizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.

Maafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakiendelea na mafunzo ya OPRAS.

Sehemu nyingine ya Watendaji Wakuu
kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia mafunzo hayo.Picha Zote na
Habari na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
No comments:
Post a Comment
This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people