HATIMAYE Ndege ya kwanza ya abiria imetua katika Uwanja wa
kimataifa wa Songwe jana baada ya miaka 11 ya ujenzi wake ambao tayari
umekamilika na kugharimu Sh100 bilioni.
Akizungumza baada ya kutua ndege hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (TAA), Seleman Seleman alisema kuwa tayari uwanja wa kimataifa wa Songwe umekamilika na dunia nzima ina taarifa ya kukamilika kwa uwanja huo.
Ndege Tanzania (TAA), Seleman Seleman alisema kuwa tayari uwanja wa kimataifa wa Songwe umekamilika na dunia nzima ina taarifa ya kukamilika kwa uwanja huo.
Alisema kuwa kutokana na kukamilika kwa uwanja
huo, tayari ofisi za mamlaka hiyo imeshahamia katika uwanja huo na
kuanza shughuli zake rasmi huku uwanja wa zamani ukifungwa rasmi na
hakuna ndege yoyote itakayoweza kutua katika uwanja huo.
“Tumeanzisha historia mpya kwani dunia inafahamau
kwa sasa kuna uwanja wa kimataiafa wa Songwe, upo wazi umekamilika na
umeanza kutumika rasmi leo(jana),”alisema
Alisema kuwa uwanja wa Songwe wa kimataifa ni kati ya viwanja vikubwa viwili kujengwa baada ya uhuru ukitanguliwa na uwanja wa Mkoa wa Kilimanjaro kwani viwanja vingine vimekuwa vikifanyiwa marekebisho.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mkuu
wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro alisema, aliwataka wananchi wa
Mkoa wa Mbeya kujiandaa kutumia uwanja huo kwa kuongeza kipato chao na
kuinua uchumi wa mkoa.
Alisema kuwa wakazi wa Mbeya wanapaswa kuzalisha
kwa wingi maua na matunda kwa nia ya kuinua uchumi. wa mkoa huo na uweze
kukua, “Tusiutumie uwanja huu kwa lengo la kusafiria pekee”alisema na
kuongeza:
“Uwanja wa Songwe ni fursa muhimu kwa wakazi wa
Mkoa wa Mbeya na mikoa jirani, kwani utaweza kuwasaidia katika kuongeza
pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kutokana na uwanja huo kuwa
wa kimataifa ambapo shughuli mbali mbali za kiuchumi zitafanyika
kutokana na uwanja huo,”alisema.
No comments:
Post a Comment
This is a public viewable website, post something that is not harmful to other people